Ana umri wa miaka miwili tu,lakini anavuta pakti zima la sigara kwa siku.Huyo ni Tong Liangliang,mkazi wa mji wa Tianjin nchini China.Dogo huyo anaaminika kuwa ndio mvuta fegi mdogo zaidi duniani,at least miongoni mwa waliojitambulisha kama watumiaji wa tumbaku.
Tong alianza kuvuta fegi akiwa na umri wa miezi 18 baada ya baba yake kumpatia mche kwa minajili ya kupunguza maumivu ya henia aliyozaliwa nayo dogo huyo.Kwa sasa hakuna dalili za yosso huyo kuachana na sigara kwani amekataa katakata ushauri wa kumtaka a-quit.Pia kiserengeti boy hicho hakioni aibu kuomba sigara pindi kikutanapo na mvutaji mwingine,na husononeka anaponyimwa sigara.
Mwaka 2005,mkazi mmoja wa China alituma maombi kwenda Kitabu cha Rekodi za Guinness akitaka atambuliwe kama mtu aliyeanza uvutaji sigara akiwa na umri mdogo zaidi (duniani),ambapo alianza kuvuta fegi akiwa na miaka mitatu.Japo ombi lake lilikataliwa kwa minajili kwamba "rekodi" hiyo ingechochea tabia mbaya,ni dhahiri kwamba hata ingekubaliwa ingekumbana na upinzani kutoka kwa Tong.
CHANZO: Finchannel.com
0 comments:
Post a Comment