Tuesday, 9 June 2009

Kukua kwa teknolojia kuna faida na hasara zake.Kuna nyakati faida huwa kubwa kuliko hasara,na kinyume chake.Kuna nyakati faida huwa kubwa zaidi kwa eneo au sekta flani na hasara kuwa kubwa zaidi kwenye eneo/sekta nyingine.Na ndivyo ilivyo kwa athari za teknolojia ya intaneti kwa "boksi la uzembe" (runinga au televisheni).

Ni dhahiri kwamba kinachoifanya intaneti "iipige bao" runinga ni nafasi ya mtumiaji katika kutumia chombo husika.Chukua mfano huu: unataka kutafuta nafasi za masomo na/au ufadhili sehemu mbalimbali.Unajua mahala mwafaka pa kwenda ni kwa Da Subi.Unafika hapo,unaambiwa "scholarships zitaletwa kwenu saa 2 kamili usiku"!Mfano huo wa kufikirika unasaidia kuonyesha ni kwa namna gani runinga imeendelea kuhodhi uhuru na wepesi wa kupata na kutafuta habari.Kwa upande mwingine,kwa kutumia mfano huohuo,mtumiaji ana uhuru wa kwenda moja kwa moja kwenye tovuti ya Da Subi,au ku-google maneno kama "nukta 77","Subi","Scholarships",nk.


Kingine kinachoikwaza runinga ni namna watumiaji wanavyoweza "kujichanganya" (sio kuwa confused bali namaanisha interactivity).Japo teknolojia ya runinga inajitahidi kwenda na kasi hiyo ya "kujichanganya",kwa mfano kwa kukaribisha maoni yanayoweza kusomwa "laivu",kupiga kura kwenye vipindi kama Big Borther,American Idol,nk,au kutuma video na picha kama ilivyo kwa i-Report ya CNN,ukweli unabaki kuwa maendeleo hayo ni "cha mtoto" ukilinganisha na internet inavyowezesha mambo kwenye social networks kama facebook,myspace,nk.




Kama hiyo haitoshi,mtumiaji wa intaneti anaweza kuangalia runinga pasipo na matatizo (ali mradi kompyuta yake iwe na vifaa stahili na spidi mwafaka) ilhali ku-access intaneti kwenye televisheni bado ni tatizo japo baadhi ya vinajitahidi kumwezesha msomaji kutembelea kurasa flani flani.Tatizo bado linabaki kuwa kurasa hizo ni chache na zinaamuliwa na kituo husika


Wanaopenda uhuru wa kufanya mambo wanavyo taka wao wanaiona teknolojia ya runinga kama ya "kidikteta" ambapo ushiriki wa mtumiaji ni mdogo zaidi kulinganisha na ule wa kwenye intaneti.Unapoingia mtandaoni,huhitaji kuangalia "ratiba ya vipindi" (kama ilivyo kwenye tv) bali una uhuru wa kuzurura upendavyo.


Kwa mujibu wa kituo cha runinga cha Channel 4 cha hapa Uingereza,idadi ya vijana wanaoangalia televisheni imekuwa ikishuka kwa kasi kubwa kulinganisha na matumizi yao ya intaneti.Na pengine katika kutambua hilo ndio maana hata gwiji la umiliki wa vyombo vya habari,Rupert Murdoch,aliamua kununua tovuti ya "kujichanganya" ya Myspace.Tajiri huyo ni mmiliki wa Fox News,Wall Street Journal,New York Times,Sky na mlolongo wa vyombo vya habari duniani anaamini kuwa future ya sekta ya habari iko kwenye intaneti.

Unaonaje?

0 comments:

Post a Comment

Categories

Unordered List

Sample Text

Blog Archive

Labels

Follow Us on FaceBook

Popular Posts

Recent Posts

Recent Comments

Recent Premium Themes

Your Links

Flickr

Powered by Blogger.

Blog Archive

Followers

Download

Your Links

Blogger Tricks

Popular Posts

Recent Posts

Text Widget