Hoja yake ya msingi ni kwamba hawezi kujiuzulu katika kipindi hiki ambacho Uingereza,kama ilivyo kwa mataifa mengi ulimwenguni,inakabiliwa na msukosuko wa uchumi.
Pamoja na msimamo huo,leo Brown ametangaza mabadiliko (reshuffle) katika baraza lake la mawaziri ambapo baadhi ya "mastaa" wameendelea na nyadhifa zao,notably "Waziri" wa Mambo ya Nje (Foreign Secretary) David Miliband (pichani chini)na "Waziri wa Fedha" (Chancellor of the Exchequer) Alistair Darling (pichani chini)Mwanasiasa ambaye jina lake limekuwa likihusishwa na kuchukua nafasi ya Brown pindi "mapinduzi" yakifanikiwa,Alan Johnson,amehamishiwa "Wizara ya Mambo ya Ndani" (Home Office) kutoka "Wizara" ya Afya."Home Office" inatajwa kuwa "kitimoto" kwa kila anayeteuliwa kuiongoza hasa kwa vile inagusa masuala nyeti kama uhamiaji na usalama wa raia (ambapo jeshi la polisi na ishu za ugaidi ni vipaumbele).
Pia katika reshuffle hiyo,Brown amemteua mfanyabiashara tajiri,Sir Allan Sugar,kuwa "enterprise tsar" (sijui tafsiri yake kwa Kiswahili inakuwaje!).
Sir Allan,anayefahamika zaidi kwa kibwagizo cha "You're Fired" katika kipindi alichokiasisi cha The Apprentice,sasa anakuwa Lord Sugar kutokana na wadhifa huo mpya unaomwingiza katika Bunge la Mamwinyi (The House of Lords).
Sir Allan,anayefahamika zaidi kwa kibwagizo cha "You're Fired" katika kipindi alichokiasisi cha The Apprentice,sasa anakuwa Lord Sugar kutokana na wadhifa huo mpya unaomwingiza katika Bunge la Mamwinyi (The House of Lords).
0 comments:
Post a Comment