Wednesday, 8 October 2008


Tukiweka kando usemi kwamba beauty is in the eye of the beholder,mtu mwenye sura mbaya au asiye na mvuto anaweza kujua ukweli huo sio kwa kujiangalia kwenye kioo tu bali hata pia kusikia kutoka kwa watu ambao hawana interest na uzuri au ubaya wa mtu huyo.Mwanamke au mwanaume akikupenda lazima atakuvisha kilemba cha ukoka.Kwa mantiki hiyo,the most reliable source katika kufahamu uzuri au ubaya wa mtu sio yule ampendaye (au anaye-pretend kumpenda).It goes without saying kwamba mpenzi wako akikwambia kwamba wewe ni mbaya,na hasa pale ambapo ushasikia tetesi kama hizo,inamaanisha kwamba mapenzi hayo yanaelekea ukingoni.Wajuzi wa mambo hayo wanasema kwamba too much honesty kwenye mapenzi ni hatari.

Lakini kuna habari moja njema kwa wenye sura mbaya na wasio na mvuto.Mtu anayesaka mapenzi ya dhati anahitaji mwenza ambaye hatayumba katika mapenzi.Yaani,sio habari za "usiponitaka wewe wenzio kibao wananitamani."Inaaminika kwamba watu wenye sura mbaya na wasio na mvuto wana tabia moja kuu: imani kwamba wanapopendwa ni sawa na bahati ya mtende ambayo wakiipoteza hawataipata tena.Kwa mantiki hiyo,watajitahidi kila wawezavyo kuhakikisha hawaipotezi bahati hiyo,which directly translates into kudumu kwa mapenzi.

Kuna kanuni (theory) nyingine isiyo rasmi kuhusu watu wenye mapungufu (kwa mfano wabaya,wasio kamilifu kimwili,nk).Kwamba,wanajitahidi kadri wawezavyo kufidia mapungufu hayo kwa kuwa na tabia au matendo yatakayowavutia wale ambao otherwise wangewapuuza kwa kigezo cha mapungufu hayo.Angalia watu wafupi,kwa mfano.Wengi wao ni waongeaji sana,wachangamfu na machachari.Tabia hiyo huwasaidia sana hadharani kwani husababisha ufupi wao kuwa sio ishu muhimu.

Nilisoma mahala flani kuhusu kwanini wanawake warembo sana huwa na wakati mgumu kudumu na mpenzi mmoja.Kwa upande mmoja sababu inaweza kuwa kutojiamini kwa wapenzi wao,yaani wazo kwamba siku yoyote wataporwa.Kwa upande mwingine ni tabia iliyozoeleka kwa warembo sana kwamba "ukifanya hivi nakubwaga" (hata kama sio suala la kubwagwa) kwa vile wanajiamini kwamba wana soko kubwa la wanaowatamani.Ni hadi umri unapoyoyoma ndipo wanawake wa aina hiyo huanza kushtuka kwamba "eh kumbe bado sijaolewa!"

Tatizo kubwa linalowakabili wenye sura mbaya na wasio na mvuto ni jinsi ya kuonekana ili wakutane na wapenzi-watarajiwa wao.Sio siri kwamba mwonekano wa nje umeendelea kuwa factor kubwa ya kupata au kukosa umpendaye.Upendo,huruma, "ufundi kwenye mahaba", na mambo mengine mazuri hujulikana baada ya ku-win heart ya umpendaye,havionekani kwa nje.Hata hivyo,mapenzi kama starehe ndio hujali zaidi mwonekano wa nje.Mtafuta mke au mume wa kudumu naye lazima atajitahidi kwenda mbali zaidi ya mwonekano wa nje.Kwa maana hiyo,japo inaweza kuchukua muda mrefu kwa mwenye sura mbaya na asiye na mvuto,lakini mwenye tabia maridhawa,kuonekana au kumpata wa kudmu naye,la muhimu ni kwamba uwezekano huo upo.

For all you ugly and unattractive guys and ladies out there,most important thing is never giving up hope in finding your true love and sticking to your good characters.Someone out there is looking for,not how you look,but those outstanding characters of yours.

0 comments:

Post a Comment

Categories

Unordered List

Sample Text

Blog Archive

Labels

Follow Us on FaceBook

Popular Posts

Recent Posts

Recent Comments

Recent Premium Themes

Your Links

Flickr

Powered by Blogger.

Blog Archive

Followers

Download

Your Links

Blogger Tricks

Popular Posts

Recent Posts

Text Widget