Monday, 13 October 2008

 Choo katika behewa la First Class TAZARA

Habari hii imenisikitisha sana kwa vile inanigusa binafsi.Ili nifike nyumbani Ifakara nina choices mbili ambazo zote si nyepesi.Kuna usafiri wa barabara ambao kwa hakika unahitaji moyo hasa kutokana na ubovu wa barabara kuanzia maeneo ya Ruaha/Kilombero.Kana kwamba hiyo haitoshi,wafanyabiashara wa mabasi ya abiria kwenda mikoani ni kama wameisusa barabara ya kwenda kwetu kwani takriban mabasi yote yaendayo huko ni mikweche ya daraja la kwanza.Mabasi kama Moro Best,Islam na Chimpanzee yamechoka kupita kiasi,na yanaendelea kutumika kwa vile tu  imekuwa kawaida yetu Watanzania kuvumilia mateso.Kikwazo kikubwa cha usafiri wa barabara ni msimu wa masika.Kuna eneo sugu kati ya Mang'ula na Kiberege ambapo kupita kunahitaji zaidi ya sala na trekta linalovuta mabasi yanayokwama kwenye matope.

 Kiza katika Stesheni Kuu ya TAZARA Dar es Salaam.Imagine kama stesheni kuu ni hivyo,stesheni ndogo itakuwaje!

Mkombozi wa wengi alikuwa TAZARA japo mara ya mwisho nilipotumia huduma zao (tena daraja la kwanza) nilitamani kulia:madirisha hayafungiki,taa zinawaka kwa kubembelezwa na vyoo ni kama kwenye baa za uswahilini.Ili ushuke kutoka behewani hadi kwenye platform ya stesheni ni muhimu kuwa mwanamazoezi wa short- au long-jump.Sasa ndio hata huduma hiyo ya kichovu nayo imepunguzwa ambapo kutakuwa na safari mbili tu kwa wiki,moja ya express na nyingine ya ordinary.Sishangai TAZARA kuchukua uamuzi huo kwani shirika hilo muhimu liko mahututi intensive care,hali yake ni mbaya na linasubiri kufa kifo cha kizembe siku si nyingi.

 Adha ya usafiri wa barabara kwenda kwetu Ifakara

Najua siko peke yangu ninaesononeshwa na habari hii lakini japo wanasema kilio cha wengi ni harusi ukweli unabaki kwamba Maisha Bora kwa "wana wa pakaya" yanazidi kuwa a distant pipedream.

0 comments:

Post a Comment

Categories

Unordered List

Sample Text

Blog Archive

Labels

Follow Us on FaceBook

Popular Posts

Recent Posts

Recent Comments

Recent Premium Themes

Your Links

Flickr

Powered by Blogger.

Blog Archive

Followers

Download

Your Links

Blogger Tricks

Popular Posts

Recent Posts

Text Widget