Wednesday, 22 October 2008


Barack Obama akifanikiwa kushinda urais hapo Novemba 4 atakuwa ameweka historia kwa kuwa Mweusi wa kwanza kuwa rais wa Marekani.Lakini mafanikio ya Obama yanawasumbua wachambuzi wa siasa (hususan za tabia za uchaguzi wa Marekani).Hayawasumbui kwa vile Obama na wao ni wabaguzi.La hasha,bali ni namna hisia kwamba Bradley effect ingemwangusha zinavyoelekea kuwa wrong.

Nilishakiri katika post yangu moja huko nyuma kwamba awali nilitamani Hillary Clinton apitishwe kuwa mgombea wa Democrats.Sababu yangu kuu ilikuwa ni katika hofu kwamba Obama angeshinda nomination basi Weupe wangeungana bila kujali itikadi zao kuhakikisha mtu mweusi haingii White House.Baada ya kumbwaga Hillary,nililazimika kukubaliana na busara za stadi za siasa kwamba lolote linawezekana katika fani hiyo.

Tukirejea kwenye kinachowasumbua wachambuzi wa siasa ni namna Bradley effect inavyoelekea kushindwa kuwa na impact kwa Obama,hasa kipindi hiki ambacho sio tu anapambana na Mweupe bali Mweupe kutoka chama cha weupe wahafidhina (Republican).Kuna wanaoamini kwamba Bradley effect ni uzushi (myth) wa aina flani.I dont.Lakini kama sio myth basi kwanini Obama anazidi kupaa kwenye opinion polls?

Binafsi nadhani hii ni REVERSE BRADLEY EFFECT.Yaani,wapiga kura Weusi hawaonyeshi dhamira zao hadharani (kwa wanaochukua opinion polls) kwamba watamsapoti Mweusi mwenzao.Kwa lugha nyingine,wanashusha matarajio ya support ya Weusi kwa Mweusi mwenzao.Lakini kwa vile Weusi ni wachache Marekani,na hata kama wangefanya nacho-hypothesize hapo juu bado wasingeweza kuifanya hali kuwa kama ilivyo sasa,nachoamini zaidi ni tabia "mpya" ya Weupe kudai hadharani kuwa hawajaamua wampigie kura nani (undecided) au Weupe (hasa wa Republicans) kuongopa hadharani kwamba wanamsapoti McCain ilhali dhamira na sapoti yao ni kwa Obama.

Weusi wa Obama ni issue kwenye uchaguzi huu,nami ni muumini wa hoja kwamba kama Obama angekuwa Mweupe basi muda huu tungeshafuta uwezekano wa McCain kuwa rais hapo Novemba.Kwanini nasema hivyo?Wamarekani wengi wamechoshwa na Republicans na uhafidhina kwa ujumla.Bush ameendelea kuwa one of the most unpopular US presidents ever,na Democrats wanaonekana kama ndio watakaoleta ufumbuzi wa matatizo ya Marekani.Sababu zote hizo ni tosha kumfanya mgombea anayekubalika wa Democrats kuwa mbali sana kwenye kura za maoni.Kwanini Obama anamwacha McCain kwa wastani wa kura 10 tu?Jibu la haraka ni Weusi wake.

Whether Bredley effect ni hype au ndio ujio wa Reverse Bredley effect itajulikana baada ya exit polls hapo Novemba 4.However,no matter what happens to Obama,alipofika ni historia tosha,japo itanoga zaidi akishinda kiti hicho.

0 comments:

Post a Comment

Categories

Unordered List

Sample Text

Blog Archive

Labels

Follow Us on FaceBook

Popular Posts

Recent Posts

Recent Comments

Recent Premium Themes

Your Links

Flickr

Powered by Blogger.

Blog Archive

Followers

Download

Your Links

Blogger Tricks

Popular Posts

Recent Posts

Text Widget