Wednesday, 29 October 2008

BARAZA Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) mkoa wa Dar es Salaam limewaonya maaskofu wa Jumuiya za Kikristo Tanzania (CCT) kutoitisha Serikali katika suala la kujiunga na Jumuiya ya Kiislamu (OIC) na kuanzisha Mahakama ya Kadhi nchini wakitishia kuwa kitendo hicho ni uhafidhina na ugaidi. 

Tamko hilo limetolewa na Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam, Sheikh Mussa Salum kwa waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, mara baada ya kikao cha masheikh na maimamu wa mkoa huo kujadili pamoja na mambo mengine, kauli ya maaskofu hao. 

"Waislamu tunasema suala la Tanzania kujiunga ama kutojiunga ni suala la Serikali ya Tanzania kwa maslahi ya wananchi wote," alisema Sheikh Salum. 

Sheikh Salum aliongeza kuwa suala la Mahakama ya Kadhi ni haki ya Waislamu wa nchini na wala halina mjadala kwa kuwa haliwahusu watu wa dini nyingine na kwamba mifano mingi ipo katika nchi mbalimbali juu ya kuwepo kwa mahakama hizo. 

"Mahakama hizi zilikuwepo tangu ukoloni, hivyo hili siyo suala la kuomba kuanzishwa kwake bali tunaiomba Serikali izirejeshe," alisema. 

Pia masheikh na maimamu hao walihoji uhalali wa kuwepo kwa Balozi wa Vatican hapa nchini kuwa anawakilisha nchi gani na kuliita kuwa suala hilo limegubikwa na udini lakini Waislamu hawakuwa wakihoji. 

"Tunawaonya maaskofu kuacha kuishinikiza Serikali mara kwa mara kuhusu masuala yanayohusu Waislamu na waache kupandikiza chuki kwa waumini wao juu ya suala la OIC na Mahakama ya Kadhi na waumini wa dini ya kiislamu kwa ujumla," alisema. 

Mwishoni mwa wiki iliyopita maaskofu 64 wa makanisa mbalimbali nchini walisaini waraka wa kumpinga Waziri Membe aliyekaririwa awali akiwataka Watanzania kutoogopa kujiunga na OIC kwani ni jumuiya yenye maslahi mazuri ya kiuchumi kwa taifa, akikariri utafiti uliofanywa na Serikali. 

Tayari BAKWATA makao makuu imeshatangaza kuitisha mkutano wa hadhara utakaofanyika kwenye viwanja vya Kidongo Chekundu kesho kueleza msimamo wake kuhusu suala hilo.

CHANZO: Majira

Related Posts:

  • TUSIPOKUWA MAKINI SUALA LA OIC NA KADHI LITATUFIKISHA PABAYAMoja ya matokeo (findings) katika utafiti wangu wa shahada ya uzamifu (ambao unahusu harakati za Waislamu nchini Tanzania) ni mtizamo wa asilimia kubwa ya Waislamu kwamba hawatendewi haki.Wapo wanaoona kuwa chanzo cha tatizo … Read More
  • CCM "YARUKA KIMANGA" KUHUSU ISHU YA OICCCM haihusiki na OIC-Msekwa27 Oct 2008By Waandishi Wetu, Dar na ZanzibarChama Cha Mapinduzi (CCM) kimeukana mpango wa Tanzania kujiunga na Jumuiya ya Kimataifa ya Kiislamu (OIC) na kusema kwa hilo vyombo vya habari na maaskof… Read More
  • SAKATA LA OIC LAENDELEA,MASHEHE WADAI MSIMAMO WA MAASKOFU NI UGAIDIBARAZA Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) mkoa wa Dar es Salaam limewaonya maaskofu wa Jumuiya za Kikristo Tanzania (CCT) kutoitisha Serikali katika suala la kujiunga na Jumuiya ya Kiislamu (OIC) na kuanzisha Mahakama ya Kadh… Read More
  • MAASKOFU WAKARIPIA MATAMSHI YA MEMBE KUHUSU OICNa Peter EdsonJUMUIYA ya Kikristo Tanzania (CCT) imemuonya Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe kuwa kauli zake kuhusu kujiunga na Jumuiya ya Kimataifa ya Nchi za Kiislamu (OIC) zinaweza kusababis… Read More
  • PENGO,MEMBE WAJADILI OICPicha kwa hisani ya BONGOPICHAWAKATI serikali ikishutumiwa na viongozi wa madhehebu ya Kikristo, juu ya Tanzania kutaka kujiunga na Jumuiya ya nchi za Kiislamu (OIC) na kuanzishwa kwa Mahakama ya Kadhi nchini, Waziri wa Mambo… Read More

0 comments:

Post a Comment

Categories

Unordered List

Sample Text

Blog Archive

Labels

Follow Us on FaceBook

Popular Posts

Recent Posts

Recent Comments

Recent Premium Themes

Your Links

Flickr

Powered by Blogger.

Blog Archive

Followers

Download

Your Links

Blogger Tricks

Popular Posts

Recent Posts

Text Widget