Kuna nyakati huwa napatwa na hisia kwamba baadhi ya makampuni makubwa huko nyumbani (hasa ya kigeni) yanachuma faida kubwa kupita kiasi to an extent of kukurupuka na sherehe zisizo na vichwa wala miguu.Kwa mujibu wa gazeti la Tanzania Daima,kampuni ya Multichoice leo itafanya sherehe za kumpongeza mshiriki wa kwanza kutolewa kwenye Big Brother ya Afrika,Latoya Lyakurwa wa Tanzania.Hivi anapongezwa kwa upuuzi aliofanya ndani ya jumba hilo au kwa kuwa wa kwanza kutolewa katika mashindano hayo?Kama jibu ni ndio kwa swali la kwanza basi huu ni ufisadi wa kimaadili (moral corruption) na kama jibu ni ndio kwa swali la pili basi yayumkinika kuamini kwamba Multichoice wana fedha za kuchezea (pengine kutokana na faida kubwa wanayopata) kupongeza a loser badala ya winner kama ilivyozoeleka.Yaani hata kushindwa nako kunaambatana na sherehe ya pongezi!?
Friday, 3 October 2008
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Its like a second grade soccer game...everybody gets a trophy.
ReplyDelete