Thursday, 2 October 2008

Mdahalo kati ya running mates wa vyama vya Democrat na Republican,Joe Biden na Sarah Palin,respectively,umemalizika hivi punde.Uchambuzi wa haraka haraka unaonyesha kuwa Palin amejitahidi kufanya vizuri kuliko ilivyotarajiwa.Matarajio kwamba Palin angefanya vibaya yalitokana na performances zake za hivi karibuni katika mahojiano (ya nadra) na wanahabari.Hofu zaidi ilikuwa ni kweli u-kilaza wake kwenye mambo mbalimbali.Kwa upande wa Biden,huku akitarajiwa kuutumia vizuri uzoefu wake wa muda mrefu kwenye ulingo wa siasa,hofu zaidi ilikuwa ni katika tabia yake ya "kusema ovyo" na kuwa gaffe-prone.Hata hivyo,uchambuzi wa awali unaonyesha kuwa Biden amefanya vizuri sana katika mdahalo huo,kiasi cha mchambuzi mmoja kudai kwamba it was his best ever performance.

Kwa upande mwingine,Palin ameonekana kama amethibitisha kwamba McCain hakufanya kosa kumchagua yeye kuwa running mate wake lakini ameshindwa kum-portray McCain kama mtu anayefaa zaidi  kuwa rais kuliko Barack Obama.Lakini Biden,pengine kwa kuhofia kuonekana kuwa ni sexist dhidi ya Palin,ametumia muda mwingi kuonyesha kwanini Obama anafaa zaidi kuwa rais kuliko McCain na wakati huohuo kuonyesha kuwa tiketi ya McCain-Palin ni mwendelezo mwingine wa miaka minane ya George W Bush.

Kiujumla,na kama ilivyotarajiwa na wengi,Biden ameonekana kuwa msindi katika mdahalo huo japo hilo haliwezi kukubalika among the Republicans.Pia matokeo ya awali ya kura kadhaa za maoni baada ya mjadala huo zinaonyesha ushindi mzuri kwa Biden hasa miongoni mwa undecided voters.


0 comments:

Post a Comment

Categories

Unordered List

Sample Text

Blog Archive

Labels

Follow Us on FaceBook

Popular Posts

Recent Posts

Recent Comments

Recent Premium Themes

Your Links

Flickr

Powered by Blogger.

Blog Archive

Followers

Download

Your Links

Blogger Tricks

Popular Posts

Recent Posts

Text Widget